WENYEJI
Yanga SC, leo wameanza vibaya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki
na Kati, Kombe la Kagame baada ya kufungwa mabao 2-1 na Gor Mahia ya
Kenya katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kipigo
cha Yanga SC leo kwa kiasi kikubwa kilichangiwa na kucheza pungufu kwa
zaidi ya dakika 65, kufuatia mshambuliaji wake, Mzimbabwe Donald Ngoma kutolewa kwa kadi nyekundu mapema kipindi cha kwanza.
Yanga
waliuanza vizuri mchezo huo na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika
ya tano tu kupitia kwa Ngoma aliyepiga mpira mrefu kama krosi kutoka
upande wa kushoto na kutinga nyavuni, huku beki Harun Shakava
akiusindikiza kwa macho.
Winga
Simon Msuva alichangia kuwatibulia hesabu za kuokoa Shakava na kipa
wake, Boniface Olouch kutokana na kuifuatilia vizuri krosi ya Ngoma hadi
inatinga nyavuni.
Bao
hilo halikudumu sana, kwani Gor Mahia walifanikiwa kusawazisha dakika
ya 18 kupitia kwa na Dirkir Glay aliyepiga shuti kali la mpira wa adhabu
lililomshinda kipa Ally Mustafa ‘Barthez’.
Faulo hiyo ilitolewa baada ya beki wa kulia, Juma Abdul kumuangusha Godfrey Walusimbi nje ya boksi.
Refa
Ssali Mashood alimtoa nje kwa kadi nyekundu Mzimbabwe, Ngoma baada ya
kumuonyesha kadi ya pili ya njano kufuatia kumsukuma Shakava wa Gor
baada ya kumpamia na mpira hadi nje ya Uwanja dakika ya 25.
Yanga
SC walitulia baada ya kumpoteza Ngoma aliyeondoka uwanjani analia na
kuanza kucheza kwa tahadhari kuwanyima nafasi Gor, hali ambayo ilisaidia
dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizike timu hizo zikiwa
zimefungana 1-1.
Kipindi
cha pili, Gor Mahia waliingia na mashambulizi ya kulazimisha na
kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya kwanza tu kupitia kwa
mshambuliaji wake, Michael Olunga, aliyewapiga chenga mabeki wa Yanga
kabla ya ‘kufyatua’ shuti lililompita Barthez.
Yanga
SC walipoteza nafasi nzuri ya kupata sare dakika ya 73, baada ya
Nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kumdakisha mkwaju wa penalti kipa
Oluoch, kufuatia Shakava kuunawa mpira kwenye boksi.
Katika
mchezo huo uliohudhuriwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Amolo
Odinga, kwa ujumla, Yanga SC iliathiriwa na kucheza pungufu.
Kikosi
cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul/Joseph Zuttah
dk75, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’,
Mbuyu Twite, Simon Msuva/Kpah Sherman dk69, Haruna Niyonzima, Amisi
Tambwe, Donald Ngoma na Deus Kaseke/Salum Telela dk84.
Gor
Mahia; Boniface Olouch, Mussa Mohammed, Sibomana Abouba, Harun Shakava,
Kari Nzigiyimana, Dirkir Glay, Khalid Aucho/Erick Ochieng dk89, Godfrey
Walusimbi/Ronald Omino dk86, Innocent Wafula/Enock Agwanda dk86, Medie
Kagere na Michael Olunga.
Wakati huohuo APR
ya Rwanda imeanza vyema michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na
Kati, Kombe la Kagame kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Al Shandy ya Sudan
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika
mchezo huo wa Kundi C, bao pekee la APR lilifungwa na kiungo Bizimana
Djihad, dakika ya 64 kwa shuti kali baada ya kupasua katikati ya Uwanja
na baada ya kupata upenyo.
Kiungo
huyo aliyesajiliwa mapema mwezi huu kutoka kwa mahasimu, Rayon Sport
ili kuziba pengo la Jean Baptiste Mugiraneza aliyehamia Azam FC, ni
mtoto wa dada wa kiungo wa Yanga SC, Haruna Niyonzima, ambaye pia
aliwika Rayon na APR kabla ya kuja Tanzania.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumamosi, 18 Julai 2015
YANGA YAPOKEA KICHAPO,APR YAFANYA KWELI
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni