STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 7 Agosti 2015

BAADA YA KUMALIZIKA MICHUANO YA KAGAME, HIKI NDICHI KIKOSI BORA CHA MASHINDANO HAYO...

Tokeo la picha la cecafa kagame cup 2015
MICHUANO ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati Kombe la Kgame imamealizika Jumapili na Azam FC kuwa mabingwa wapya kwa kunyakua ubingwa huo kwa mara ya kwanza tangu ilipoanza kushiriki michuano hiyo iliyokuwa inafanyika kwa mara ya 40.
1.Aishi Manula. AZAM FC
Huyu ni kipa namba moja wa Azam ambaye amedaka mechi tano kati ya sita ilizocheza timu hiyo hadi kufika fainali kitu pekee kinachomfanya kuwemo kwenye kikosi hiki bora nikutoruhusu bao hata moja kwenye michuano licha ya kuwa katika wakati mgumu wa kuokoa michomo ya karibu kwenye baadhi ya mechi ikiwemo ile ya robo fainali alipookoa penati nusu fainali dhidi ya KCCA na hata mchezo wa fainali dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.
2.Karim Nizigiyimana. GOR MAHIA
Beki wa kulia wa washindi wa pili wa michuano ya Kagame 2015 Gor Mahia ambaye ameonyesha uwezo mkubwa wa kuipigania timu yake tangu mechi ya kwanza hadi fainali ambapo mara zote alikuwa akipada mbele kusaidia mashambulizi na katika mechi saba alizo cheza ameweza kupiga pasi nne zilizo zaa mabao yaliyofungwa na Michael Olunga na Medie Kagere.
3.Hajji Mwinyi. YANGA
Licha ya kukosa penati iliyoitoa Yanga kwenye mashindano ya mwaka huu kwenye mchezo war obo fainali dhidi ya mabingwa Azam FC, lakini beki huyo aliyekuwa anaichezea timu hiyo kwa mara ya kwaza alitoa mchango mkubwa katika mechi zote tano alizoichezea Yanga akitokea beki wa kushoto mara nyingi alikuwa akifanya kazi mbili kwa wakati mmoja wa kuzuia na kwenda mbele kupiga krosi kwa washambuliaji wake Amisi Tambwe na Donald Ngoma.
4.Manirakiza Aruna. LLBA FC
Nibeki aliyetoa mchezo mkubwa kwa timu yake ya LLBA FC ya Burundi kwani licha ya kutolewa kwenye hatua ya makundi baada ya kufungwa na APR katika mchezo wa mwisho lakini Aruna alionyesha kiwango cha juu kilichomfanya aingie kwenye orodha hii ya kikosi bora cha michuano ya Kagame 2015.
5.Pascal Wawa. Azam FC
Raia wa Ivory Coast ambaye ametoa mchango mkubwa kwa Azam hadi kufikia kutwaa ubingwa huo wa kwanza aliweza kupambana vizuri na washambuliaji hatari akina Michael Olunga na Amissi Tambwe wa Yanga na kuweka historia ya timu yake kumaliza michuano bila kufungwa hata bao moja.
6. Aucho Kgalid. Gor Mahia
Kiungo bora aliyefanya kazi kubwa ya kuzuia mashambulizi ya timu pinzani yaliyokuwa yanaelekezwa kwenye llango la timu yake na uhodari wa kiungo huyo ulitokana na uwezo na nguvu alizokuwa nazo huku mara kadhaa akisogea mbele kusaidia mashambulizi.
7.Birungi Michael. KCCA
Winga hatari wa KCCA ya Uganda ambaye amechangia kwa kiasi kikubwa timu hiyo kumaliza nafasi ya tatu ya michuano hiyo mikubwa Afrika Mashariki na Kati, kocha Mike Mutebi atakuwa anajilaumu sana kwa kumuanzisha benchi katika mechi za awali Birungi ndiye aliyefunga bao la kwanza katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Al Khartoum kuwania nafasi yatatu.
8.Haruna Niyonzima. Yanga
Amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu hiyo tangu alipojiunga nayo msimu minne iliyopita akitokea APR ya Rwanda Niyonzima licha ya kuchelewa kujiunga na wenzake kujiandaa na michuano hiyo lakini alikuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha kocha Hans van der Pluijm kutokana na uwezo wake wa kuichezesha timu na kupiga pasi za mwisho licha timu hiyo kutolewa na Azam kwa penati hatua ya robo fainali.
9.Michael Olunga. Gor Mahia
Hakuna ubishi huyu ndiye mshambuliaji aliyefanya vizuri kwenye michuano hii akifunga mabao matano na kuibuka mfungaji bora amechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Gor Mahia kwenye michuano ya 2015 ndiye mchezaji pekee aliyekuwa gumzo na hasa kiwango alichokionyesha kwenye pambano la ufunguzi dhidi ya Yanga ambapo alifunga bao la ushindi
Baada ya hapo Olunga alitajwa kuwaniwa na timu tatu zenye ushindani Tanzania za Yanga,Azam na Simba.
10.Salah Eldin Osman. Al Khartoum
Nahodha wa Khartoum ambaye kwenye michuano ya Kgame mwaka huu ameifungia timu yake mabao manne na kumaliza nafasi ya pili nyuma ya Olunga Salah licha ya mabao hayo lakini ameonyesha kiwango cha juu na kuisaidia timu yake hadi kucheza robo fainali baada ya kuifunga timu ngumu ya APR mabao 4-0.
11.Godfrey Walusimbi.Gor Mahia
Winga machachari wa washindi wa pili wa michuano ya Kombe la Kgame mwaka huu ametoa mchango mkubwa kwa timu yake ikiwemo kufunga mabao mawili katika mchezo dhidi ya Telecom ya Djibout.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox