Kwa mujibu wa John High shabiki wa klabu ya West Ham United ya Uingereza amekiri kupitia ukurasa wake wa twitter kuwa ni miaka 52 sasa klabu ya West Ham United haijawahi kuifunga klabu ya Liverpool katika uwanja wake wa nyumbani Anfield.
John ambaye ni shabiki wa damu wa West Ham United aliahaidi kupitia account yake ya twitter kuwa endapo West Ham itamfunga Liverpool katika uwanja wake wa nyumbani Anfield atachora tattoo ya matokeo hayo mwilini mwake hivyo baada ya ushindi wa goli 3-0 John amechora tattoo hiyo na majina ya walio funga magoli na muda.
Klabu ya West Ham United mara ya mwisho kuifunga klabu ya Liverpool katika uwanja wake wa nyumbani Anfield ni mwaka 1963 hivyo mashabiki wa klabu hiyo wengi wao August 29 ni siku ya kihistoria kwao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni