Wilshere, mwenye Miaka 23, aliumizwa Mazoezini Jumamosi iliyopita ikiwa ni Siku moja tu kabla Arsenal hawajaifunga Chelsea 1-0 huko Wembley na kutwaa Ngao ya Jamii.
Ingawa imethibitishwa kuwa Kiungo huyo wa England hatahitaji Operesheni lakini kuumia huko kutamweka nje kwa kipindi kitakachofikia hadi Miezi Miwili na hivyo kuukosa mwanzo wa Msimu mpya wa Soka wa England unaoanza Wikiendi hii.
Pigo hilo kwa Arsenal ni mwendelezo wa Majeruhi kabakaba yanayomwandama Wilshere ambae Msimu uliopita alikuwa nje kwa Miezi Mitano baada ya kuumia enka yake ya Kushoto na kufanyiwa Operesheni.
Tangu aanze Soka lake, Wilshere ameshafanyiwa Operesheni katika Enka zake zote mbili.
Wilshere-Na Majeruhi yake Arsenal:
Oktoba 2009: Wiki 5 nje
Julai 2011: Miezi 15
Machi 2013: Wiki 6
Mei 2013: Wiki 7
Oktoba 2013: Wiki 2
Januari 2014: Wiki 2
Machi 2014: Miezi 2
Oktoba 2014: Wiki 2
Novemba 2014: Miezi 5
Agosti 2015: Miezi 2

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni