KOCHA
wa zamani wa Yanga SC, Mbelgiji Tom Saintfiet amemfukuza kabisa
mshambuliaji wa Tottenham, Emmanuel Adebayor katika timu ya taifa ya
Togo.
Saintfiet
aliyeipa Yanga SC ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati mwaka 2012,
ambaye sasa anaifundisha Togo, amesema hatamuita tena kikosini Adebayor
baada ya kukataa wito wa kujiunga na kikosi kilichomenyana na Djibouti mwishoni mwa wiki katika mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika.
Na
hiyo inakuja baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kutemwa
katika kikosi cha wachezaji 25 wa -Tottenham watakaocheza Ligi Kuu ya
England msimu huu.
Emmanuel
Adebayor (kulia) ameendelea kuogelea kwenye bahari ya matatizo, baada
ya kocha wa Togo, Tom Saintfiet kumfukuza moja kwa kikosini mwake
Saintfiet amesema; "Kama unatoka na mwanamke ambaye hana majibu sahihi, unapaswa kutaafuta mwanamke mwingine,"amesema Saintfiet ambaye ameshangaa Adebayor kushindwa kutuma hata meseji au email kujibu wito wake timu ya taifa.
Adebayor
alicheza na kufunga bao katika mchezo wa kwanza kufuzu AFCON dhidi ya
Liberia Juni na hiyo ilikuwa mara yake ya mwisho, kabla ya kusema
amesikitishwa na kitendo cha Saintfiet kumpokonya Unahodha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni