Klabu ya Chelsea ya Uingereza
imeonyesha muonekano wa uwanja wao mpya ambao hadi mwaka 2020
inaripotiwa ujenzi wa uwanja huo utakuwa umekamilika. Bado mashauriano
yanaendelea kuhusiana na wakazi wa eneo husika utakapo jengwa uwanja
huo.
Mpango wa mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich ni kutumia pound milioni 500 katika ujenzi wa uwanja huo ili uwe biashara tofauti inayojitegemea mbali na Chelsea. Ujenzi huo ambao unatarajiwa kuanza baada ya miezi 9 kutokea sasa utaifanya klabu ya Chelsea kuhama uwanja wao wa Stamford Bridge na kutumia Uwanja wa Wembley kwa kipindi cha misimu mitatu.
Ujenzi huo wa Uwanja mpya wa Stamford Bridge utakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000 sawa na uwanja wa Taifa wa Dar Es Salaam, ambapo uwanja wa sasa wa Chelsea unachukua watu wasio zidi 41,000.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni