

- Kevin De Bruyne jamaa aliwahi kucheza Chelsea bila mafanikio na kuishia kupelekwa kwa mkopo katika vilabu kadhaa na baadae kuuzwa Wolfsburg ya Ujerumani, Lakini sasa amesajiliwa na Man City kwa dau la pound milioni 54 akitokea Wolfsburg na anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji ghali Uingereza.


- Luis Suarez ametokea katika familia ya kimasikini, kuna wakati aliwahi kukiri kuwa alikuwa akicheza mpira peku peku na juani, lakini leo hii ni moja kati ya wachezaji muhimu katika safu ya ushambuliaji ya FC Barcelona na timu yake ya taifa ya Uruguay.


- Steven Gerrard alianza kucheza soka katika klabu ya Whiston Juniors na baadae maskauti wa Liverpool wakamuona na kumsajili katika Academy yao akiwa na umri wa miaka 9. Amewahi kufanya majaribio katika vilabu kadhaa wakati akiwa na miaka 14 ila haikuwa rahisi kufanikiwa kwa wakati huo, kwa sasa anacheza klabu ya LA Galaxy ya Marekani.



- Thiago Silva na David Luiz walianza kuingia katika headlines kwa uhodari wao katika michuano ya kombe la mabara wakiunda pamoja safu ya ulinzi imara kwa timu yao ya taifa ya Brazil . Hawa walikuwa pamoja na kuota pamoja kuwa wachezaji mahiri, sasa wanacheza pamoja katika klabu ya PSG baada ya kila mmoja kuangaika katika timu mbalimbali.
David Luiz kushoto na Thiago Silva upande wa kulia


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni