MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Ufaransa, Karim Benzema jana alikuwa mchezaji pekee
aliyecheza timu hiyo ikifungwa 4-0 na Barcelona Uwanja wa Santiago
Bernabe katika La Liga kuripoti mazoezini.Mfaransa huyo aliibuka mazoezini viwanja vya Valdebebas kuungana na wachezaji ambao hawakucheza El Clasico Jumamosi akina Casemiro, Alvaro Arbeloa and na Lucas Vazquez.
Luisa Suarez alifunga mabao mawili katika ushindi huo, wakati Neymar na Andres Iniesta kila mmoja alifunga bao moja, Real ikipoteza mechi ya kwanza ya La Liga nyumbani baada ya mechi 23.
Kikosi kizima cha Real kinatarajiwa kufanya mazoezi kamili leo kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Shakhtar Donetsk


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni