TIMU za Cameroon na
Ivory Coast zimekamilisha orodha ya timu zitakazoshiriki michuano ya
Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani-CHAN itakayofanyika Rwanda
baada ya kupata ushindi mwembamba katika mechi zao za mwishoni mwa
wiki.
Cameroon walifuzu kwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Congo
huko Brazzaville baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo
wao wa mkondo wa kwanza uliochezwa wiki mbili zilizopita.
Ivory Coast
nao halikadhalika walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ghana katika
mchezo uliofanyika jijini Abdijan na kusonga mbele kwa bao la ugenini
baada ya kuchapwa mabao 2-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza
uliofanyika jijini Kumasi.
Sasa timu hizo zinaungana na Angola, Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo, Ethiopia, Gabon, Guinea, Mali, Morocco, Niger,
Nigeria, Tunisia, Uganda, Zambia na Zimbabwe ambazo zilikuwa tayari
zimeshafuzu.
Rwanda wao wamefuzu moja kwa moja kwa mwenyeji na
kukamilisha orodha ya timu zitakazochuana katika michuano hiyo ambayo
itaanza kutimua vumbi Januari16 na kumalizika Februari 7 mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni