STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 10 Novemba 2015

DEPAY AFUNGUKA MIKAKATI YAKE......................


                 


Memphis Depay amesisitiza kua mashabiki wa Manchester United
muda si mrefu watamwona katika kiwango chake baada ya kua katika wakati mgumu ndani ya wiki kadhaa.

Depay alicheza kama kawaida kwa klabu yake mwanzoni mwa msimu huu, lakini wiki za hivi karibuni amejikuta akiwa anaingia akitokea benchi.

Mholanzi huyo amedai kua aliona ni rahisi kidogo wakati anaanza, lakini ameapa kujituma kwenye uwanja wa mazoezi ili kupata tena nafasi yake ya kuanza na kikosi cha kwanza cha kocha Louis van Gaal.

"Ukweli ni ngumu unapokua benchi lakini inaenda kua safi sasa na inaenda kua bora kwenye uwanja wa mazoezi. Kwa hiyo nikipata nafasi yangu kucheza, nitaipokea," Depay aliiambia NOS.

"Nadhani vitu vingi vimebadilika. Kwa sasa nipo klabu mpya, ni level nyingine. Vitu kama hivi vina nafasi kubwa na unajitahidi kutafuta nafasi yako ni rahisi kidogo ukiwa unaanza lakini baadae nilikwama na unaweza kuona namna nilivyocheza.

"Lakini unaweza kudhani kua niko bussy na kazi na kurejea tena juu. Najisikia niko sawa na ninajitahidi kuonesha kwenye mazoezi kua ninafanya vizuri. Watu wamezoea kuniona nikifunga na hilo linakuja lazima, ilichukua muda mrefu kidogo lakini sasa utaona kiwango hicho tena."

Depay ambaye alihamia Man United akitokea PSV Eindhoven majira ya joto, amefunga goli moja pekee msimu huu wa Premier League.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox