Na kwa matokeo hayo, Liverpool nafasi ya pili katika kundi hilo, baada ya kufikisha point inane kutokana na mechi nne ilizocheza, ikiwa nyuma ya FC Sion yenye point inane.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, FC Sion ililazimishwa sare ya 1-1 na Bordeaux Uwanja wa Stade Tourbillon, bao lao wakifungiwa na Clement Chantome aliyejifunga dakika ya 90 na ushei la wageni likifungwa na Thomas Toure dakika ya 67.
Tottenham Hotspur nayo imepata ushindi mwembamba wa nyumbani wa mabao 2-1 dhidi ya RSC Anderlecht katika mchezo wa Kundi J mabao yake yakifungwa na Harry Kane dakika ya 29 na Mousa Dembele dakika ya 87, huku la wapinzani wao likifungwa na Imoh Ezekiel dakika ya 72 Uwanja wa White Hart Lane.
Spurs sasa inafikisha pointi saba baada ya mechi nne na kupanda kileleni mwa kundi hilo, wakati mchezo mwingine wa kundi hilo FK Qarabag imegawana pointi na Monaco baada ya sare ya 1 – 1 Uwanja wa Guzanli Olympic, bao lake likifungwa na Samuel Armenteros dakika ya 39, kabla ya Ivan Cavaleiro kuwasawazishia wageni dakika ya 72.
Lazio imeshinda 2-0 ugenini dhidi ya Rosenborg mchezo wa Kundi G, mabao ya Filip Djordjevic dakika ya tisa na 29 Uwanja wa Lerkendal.
mchezo mwingine wa kundi hilo, St Etienne imeshinda 3-0 dhidi ya Dnipro Dnipropetrovsk mabao ya Kevin Monnet-Paquet dakika ya 38, Robert Beric dakika ya 52 na Romain Hamouma dakika ya 65.
Borussia Dortmund imeshinda 4-0 dhidi ya FK Qabala mchezo wa Kundi C, mabao yake yakifungwa na Marco Reus dakika ya 28, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 45, Sergei Zenjov aliyejifunga dakika ya 67 na Henrikh Mkhitaryan dakika ya 70 Uwanja wa Signal Iduna Park.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, FK Krasnodar imeshinda 2-1 nyumbani dhidi ya PAOK Salonika mabao yake yakifungwa na Ariclenes da Silva Ferreira dakika ya 33 na Joao Natailton Ramos dos Santos kwa penalti dakika ya 67, huku la wageni likifungwa na Robert Mak dakika ya 90 na ushei Uwanja wa Kuban.
Fiorentina imeshinda 2-0 ugenini dhidi ya Lech Poznan katika mchezo wa Kundi J, mabao ya Josip Ilicic dakika ya 42 na Josip Ilicic dakika ya 83 Uwanja wa INEA.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, FC Basel pia imeshinda 2-0 ugenini dhidi ya Belenenses, mabao ya Marc Janko kwa penalti dakika ya 45 na Breel Embolo dakika ya 64 Uwanja wa Estadio do Restelo.
Napoli imeshinda 5-0 dhidi ya FC Midtjylland katika mchezo wa Kundi D, mabao ya Omar El Kaddouri dakika ya 13, Manolo Gabbiadini dakika ya 23 na 38, Christian Maggio dakika ya 54 na Jose Callejon dakika ya 77 Uwanja wa San Paolo.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Club Brugge imeshinda 1-0 dhidi ya Legia Warsaw, bao pekee la Thomas Meunier dakika ya 38 Uwanja wa Jan Breydelstadion.
MATOKEO MECHI ZA JANA UEFA EUROPA LEAGUE…
Rosenborg 0-2 Lazio
Athletic Club 5-1 Partizan Belgrade
Belenenses 0-2 FC Basel
Sparta Prague 1-1 FC Schalke 04
Tottenham Hotspur 2-1 RSC Anderlecht
St Etienne 3-0 Dnipro Dnipropetrovsk
Skenderbeu Korce 3-0 Sporting Lisbon
Lech Poznan 0-2 Fiorentina
Asteras Tripolis 2-0 APOEL Nicosia
Dinamo Minsk 1-2 Villarreal
Borussia Dortmund 4-0 FK Qabala
FK Krasnodar 2-1 PAOK Salonika
Club Brugge 1-0 Legia Warsaw
Celtic 1-2 Molde
Rubin Kazan 0-1 Liverpool
Napoli 5-0 FC Midtjylland
Marseille 1-0 Sporting Braga
FC Groningen 0-1 Slovan Liberec
Ajax 0-0 Fenerbahce
Viktoria Plzen 1-2 SK Rapid Wien
FC Sion 1-1 Bordeaux
FK Qarabag 1-1 Monaco
Besiktas 1-1 Lokomotiv Moscow
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni