Licha ya kuwa mwaka 2015 staa wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo kufanya mipango yake mingi na kwa asilimia kubwa kufanikiwa, miongoni mwa ishu alizofanya Cristiano Ronaldo kwa mwaka 2015 ni kuzindua movie ya maisha yake halisi, perfume, viatu vyake lakini hii sio taarifa njema kwake.
Kutoka El Economista wametangaza kuwa kampuni ya vifaa vya michezo ya kimarekani Nike imetangaza kumtaja staa wa FC Barcelona Neymar kuwa ndio staa namba moja kwa sasa anayeuza brand ya bidhaa zao, rekodi ambayo ilikuwa inashikiliwa na Ronaldo kwa miaka kadhaa ila November 27 Neymar ndio ameandikwa kumzidi Ronaldo.
Ronaldo na Neymar wote wanamkataba wa kutangaza bidhaa za Nike
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni