Ishu ya
beki Juma Nyosso aliyefungiwa miaka miwili kutocheza soka, imeibuliwa upya
baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwa na mchakato wa kupitia upya na
kujiridhisha kama hukumu hiyo ni halali au itenguliwe.
Hiyo
imekuja baada ya Ch
ama cha Wacheza Soka Tanzania (Sputanza) kuwasilisha ombi lao
la kufanyika upya kwa zoezi hilo takriban wiki moja iliyopita na TFF kupitia
Bodi ya Ligi iliyo chini ya Mtendaji Mkuu, Boniface Wambura tayari imekubaliana
na suala hilo.
Katibu Mkuu wa Sputanza, Abeid Kasabalala amesema kwamba
ombi hilo waliliwasilisha pamoja na ada ya Sh 500,000 kulingana na mwongozo
uliotolewa huku akisisItiza kuwa hiyo si rufaa bali ni kutaka kuona haki
ikitendeka kwa mujibu wa tukio lenyewe na adhabu iliyotolewa.
“Hii
adhabu iliyotolewa na kamati ya masaa 72 tunaona haijakaa sawa kwa mchezaji,
kipindi alichofungiwa ni kirefu mno kwa hiyo tumewasilisha kupitia upya tukio
na hata vifungu vya adhabu na kuhakikisha haki inatendeka.
“Imeshapokelewa
na majibu yametoka kutoka Bodi ya Ligi kuwa muda si mrefu tutakutana pande zote
ikiwezekana na mchezaji mwenyewe (Nyosso) awepo na tuangalie upya,” alisema
Kasabalala.
Akiwa anaitumikia Mbeya City, Nyosso alipewa adhabu hiyo baada ya kuingia hatiani kwa kumdhalilisha nahodha wa Azam FC, John Bocco, katika moja ya mechi za Ligi Kuu Bara msimu huu iliyopigwa Uwanja wa Chamazi, Dar na Azam ilishinda 2-1.
Chanzo: Saleh Jembe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni