GOLIKIPA wa akiba wa
Manchester City Willy Caballero ana uhakika anaweza kuziba nafasi ya Joe
Hart kama ya majeruhi ya kipa huyo namba moja wa Uingereza aliyopata
katika mchezo dhidi ya Juventus Jumatano yatamuweka nje katika mchezo wa
Ligi Kuu dhidi ya Southampton.
Hart alipata majeruhi ya msuli wa paja
katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kutolewa nje kumpisha
Caballero katika dakika ya 81 na kuna uwezekano pia wa kuukosa mchezo wa
kesho.
Akihojiwa Caballero amesema hajapenda Hart aumie lakini anapaswa
kujiandaa kwasababu hayo ndio maisha ya kipa wa akiba. Caballero
aliendelea kudai kuwa ni vizuri kucheza michezo kadhaa mfululizo lakini
hilo litategemea na jinsi hali ya Hart itakavyokuwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni