STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 27 Novemba 2015

TAIFA STARS YA BAADAE U15 YAINGIA KAMBINI

TIMU ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) imeingia kambini jana jioni katika hosteli za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam, kujiandaa na ziara ya mafunzo katika ukanda wa Afrika Mashar
iki itakayoanza Disemba Mosi mwaka huu.
 
Kocha wa timu hiyo Sebastian Mkomwa amesema vijana wote wameshawasili jijini Dar es salaam na leo wameanza mazoezi asubuhi katika uwanja wa Karume watakapokua wanajifua kila asubuhi na jioni mpaka siku ya safari.
 
Kikosi cha wachezaji 24 kimeingia kambini kujifua na ziara ya Afrika Mashariki, ambapo timu hiyo inaandaliwa kwa ajili ya kushiriki kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17, zitakazofanyika mwaka 2017 nchini Madagascar.

Timu ya Taifa ya vijana imekuwa na program ya kukutana kila mwisho wa mwezi kwa ajili ya kufanya mazoezi na kucheza michezo ya kirafiki na timu za kombani za U15 katika mikoa mbalimbali nchini, ambapo kwe mwezi Disemba itakua pamoja kwa wiki tatu katika nchi za Afrika Mashariki ikicheza michezo ya kirafiki.
 
Disemba Mosi, U-15 itasasiri kuelekea jijini Mwanza ambapo itacheza mchezo mmoja wa kirafiki na kombani ya jijini Mwanza (U17), kasha kusafiri kueleka mkoani Kigoma itakapocheza michezo miwili dhidi ya kombaini ya mkoa wa Kigoma (U17) na timu ya Taifa ya Burundi (U17).

 
Ziara hiyo itaendelea katika jiji la Kigali kwa kucheza michezo miwili dhidi ya timu ya Taifa ya Rwanda (U17), Jinja dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda (U17), Nairobi dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya (U17) na kumalizia kwa mchezo dhidi ya kombaini ya mkoa wa Arusha (U17) na kurudi jijini Dar es Salaam.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox