STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 8 Juni 2015

SIMBA NA YANGA WAMKOSA KINDA WA BURUNDI


KLABU ya Mamelodi Sundwons ya Afrika Kusini imekamilisha usajili wa kinda Mrundi, Abdul Razak Fiston  kwa Sh. Milioni 500 kutoka klabu ya Sofapaka ya Kenya, ambaye mwaka 2013 Simba na Yanga zilijaribu kumsajili.
 
Fiston mwenye umri wa miaka 23 aliichezea kwa mara ya mwisho Sofapaka jana ikimenyana na AFC Leopards na mtu aliyefanikisha mipango hiyo ni Mtanzania, Dennis Kadito aliyewahi kumpeleka Shomary Kapombe Ufaransa.
 
Rais wa Sofapaka, Elly Kalekwa amefurahia dili hilo na amemshukuru Razak kwa mchango wake kwa kipindi chote alichokuwa na klabu hiyo.
 
“Amesaini Mkataba wa miaka mitatu na tunamtakia kila la heri. Dili hilo limeigharimu Sundowns dola za Kimarekani 250,000 (Sh. Milioni 500 na zaidi), ambalo ni sahihi na haki kabisa kwa timu zote mbili," amesema Kalekwa.
 
“Tumesaini Mkataba ambao Sofapaka itakuwa ikipata asilimia 20 iwapo Sundowns itamuuza Fiston timu nyingine,”amesema.
 
Razak sasa anakwenda kugombea namba katika timu ya kocha Pitso Mosimane dhidi ya wakali kama Cuthbert Malajila, Mame Niang na Katlego Mashego msimu ujao.
 
Mwaka juzi, wakati wa michuano ya Kombe la Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Fiston aling’ara na Burundi na viongozi wa Simba na Yanga waliokuwepo Kenya walipewa taarifa za mchezaji huyo na kujaribu kumfuatilia, lakini hawakuridhishwa naye.
 
Geoffey Nyange ‘Kaburu’, Makamu wa Rais wa Simba SC na Mussa Katabaro, Mjumbe wa Kamati ya Mashindano na Usajili ya Yanga SC wote walikuwepo Kenya mwaka juzi na wakashauriwa kuhusu Fiston na wakazungumza naye kwa wakati tofauti.
 
Lakini wote baadaye walimpuuza mchezaji huyo akasajiliwa na Sofapaka ya Kenya kutoka klabu ya Lydia Ludic Academy ya Ligi Kuu ya kao Burundi, ambayo ndiyo iliyomuibua kupitia akademi yake hiyo.  
 
Kadito mwaka juzi alifanikiwa kumpatia timu ya AS Cannes ya Daraja la Nne nchini Ufaransa, beki Shomary Kapombe akiwa Simba SC na akamshauri avumilie baada ya muda atauzwa klabu za juu.
 
Lakini baada ya miezi michache Kapombe alirejea Tanzania na kujiunga na Azam FC- kwa sasa Kadito hana hamu na wachezaji wa Tanzania baada ya kitendo cha Kapombe na amehamishia msaada wake kwa wachezaji wengine wa nchi jirani wenye nia kweli ya kucheza soka ya kulipwa nchi zenye kutoa maslahi mazuri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox