DROGBA ATAKA KUINOA CHELSEA.
MSHAMBULIAJI wa zamani
wa Chelsea, Didier Drogba amesema wana makubaliano ya kurejea katika
klabu hiyo pindi atakapostaafu kucheza na anataka kuwa meneja.
Drogba
ambaye kwasasa anacheza soka lake nchini Canada, amewahi kufunga mabao
164 katika vipindi viwili tofauti alivyoichezea Chelsea. Akihojiwa
Drogba mwenye umri wa miaka 37, amesema anataka kulipa fadhila kwa klabu
hiyo ambayo ilimpa vitu vingi jambo ambalo amekubaliana na
wakurugenzi.
Mkongwe huyo aliendelea kudai kuwa anaweza kurejea klabu
hapo kuchukua nafasi yeyote kama mkufunzi wa shule ya michezo ya timu
hiyo, mshauri wa safu ya ushambuliaji, mkurugenzi wa michezo au hata
meneja.
Drogba alifunga penati ya ushindi iliyowapa taji la Ligi ya
Mabingwa Ulaya mwaka 2012 na kushinda taji la nne la Ligi Kuu katika
kipindi chake cha pili alichorejea msimu uliopita kabla ya kujiunga na
Montreal Impact inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani-MLS.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni