
Katazo hilo limetolewa na serikali ya Russia katika kipindi ambacho nchi za Urusi na Uturuki zipo katika msuguano mzito wa kisiasa.
Msuguano umetokana na ndege ya kivita ya Urusi kutunguliwa na vikosi vya Uturuki katika mpaka wa nchi hiyo na Syria Jumanne iliyopita, tukio ambalo lilichukua maisha ya rubani wakati mtu mwingine alipona na kuokolewa na wanajeshi waliokuwa katika opereshenj maalum.
Kutokana na tukio hilo, Russian imewawekea vikwazo vya kiuchumi Uturuki, vikwazo ambavyo pia vinahusisha biashara ya usajili wa wachezaji baina ya nchi hizo mbili.
Waziri wa michezo wa Urusi Vitaly Mutko aliiambia R-Sport news agency: “Ikiwa mtu yoyote anataka kusajili mchezaji kutoka Uturuki, hakutokua na uwezekano huo.”
Hata hivyo, aliongeza wachezaji wenye asili ya kituruki ambao wamekuwa wakicheza Urusi hawatohusika na katazo hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni