TIMU
ya Arsenal imeweka hai matumaini ya ubingwa, kufuatia ushindi wa mabao
2-1 dhidi ya Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku
wa jana Uwanja wa Emirates.
Ushindi huo unaifanya Arsenal iendelee kukamata nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 36, baada ya kucheza mechi 17, ikizidiwa pointi mbili na vinara Leicester City.
Manchester City inaendelea kubaki nafasi ya tatu kwa pointi zake 32 za mechi 17, wakati Tottenham Hotspur ni ya nne kwa pionti zake 29 sawa na Manchester United, zote zikiwa zimecheza mechi 17 pia.
Olivier Giroud akishangilia baada ya kuifungia bao la pii jana
Mshambuliaji wa England, Theo Walcott alianza kuifungia Arsenal dakika ya 33 Uwanja wa kwa pasi ya kiungo Mjerumani Mesut Ozil aliyemsetia pia mshambuliaji Mfaransa Olivier Giroud kufunga la pili dakika ya 46.
Sergio Aguero alirejea uwanjani jana baada ya kukosekana muda mrefu kutokana na majeruhi, lakini akacheza kwa dakika 63 tu kabla ya kumpisha Wilfried Bony baada ya kushindwa kufunga.
Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure ndiye aliyeifungia Manchester City bao la kufutia machozi dakika ya 82.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Cech, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Ramsey, Flamini, Walcott/Chambers dk88, Ozil/Oxlade-Chamberlain dk76, Campbell/Gibbs dk70 na Giroud.
Manchester City; Hart, Sagna, Otamendi, Mangala, Kolarov, Fernandinho, Toure, Delph/Sterling dk46, De Bruyne, Silva/N
avas dk73 na Aguero/Bony dk63.
MSIMAMO WA EPL;
PICHA ZA CECH,SANCHEZ NA MONREAL WAKIONESHA MAUJUZI YA KUTUMIA VYOMBO VYA MUZIKI KABLA YA MCHEZO WA MANCHESTER CITY;
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni