Mshambuliaji hatari na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta sasa ni mali ya KRC Genk ya Ubelgiji, rasmi ameondoka TP Mazembe.
Leo, Samatta amesaini mkataba wa miaka minne na nusu kuichezea Genk ambayo inapambana katika Ligi Kuu Ubelgiji.
Kupitia
mtandao wa kijamii kwenye ukurasa wake wa Instagram, Samatta
amewashuruku wachezaji wa TP Mazembe kwa ushirikiano, lakini amemshukuru
tajiri Moise Katumbi.
“Ahsante
kwa bosi wangu Katumbi kwa fursa ya kucheza ndani ya TP Mazembe hadi
leo, Kocha, wachezaji wenzangu, mashabiki na viongozi wote, muda wote
wamenipa support.
“Napenda kuwataarifu, sasa rasmi nimekuwa mchezaji wa KRC Genk,” aliandika Samatta.
HUU NDIO MTANDAO HALISI WALIVYOPOST GENK
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni