MENEJA wa Arsenal,
Arsene Wenger amethibitisha kuwa Alex Oxlade-Chamberlain anatarajiwa
kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki sita lakini hatahitaji
kufanyiwa upasuaji wa goti lake lililoumia.
Kiungo huyo aliondoka katika
Uwanja wa Emirates akiwa na magongo baada ya kugongana na Javier
Mascherano wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona
uliochezwa wiki iliyopita.
Akizungumza na wanahabari leo Wenger amesema
pamoja na kiungo huyo kukaa kwa muda wote huo lakini hatahitaji
kupanyiwa upasuaji.
Kuna uwezekano mkubwa wa Oxlade-Chamberlain kukosa
sehemu kubwa ya mechi za Ligi Kuu wakati Arsenal ikijaribu kufukuzia
taji la Ligi Kuu lakini kuna matumaini kuwa anaweza kupona kwa wakati
ili aweze kuteuliwa katika kikosi cha Uingereza kwa asjili ya michuano
ya Euro 2016.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni