Simba ilishinda tena mchezo wake wa kirafiki dhidi ya timu ya Burkina
Faso, mchezo huo uliochezwa jana jioni ulimalizika kwa Simba kupata
ushindi wa goli 5-0.
Magoli ya Simba yamefungwa na Ibrahimu Ajibu dakika ya 1 na dakika ya
35, Mussa Ndusha Dakika ya 15′ Shizya Kichuya dakika ya 55 na Said
Ndemala dakika ya 65 mchezo huu ni wa tatu kwa timu ya Simba kupata
ushindi katika michezo yote mitatu ya kirafiki aliyocheza tangua iweke
kambi mkoani Morogoro.
Imeshacheza na Timu ya Polisi Moro wakapata ushindi wa 5-0,Simba vs
Moro Kids ikashinda kwa goli 2-0. Simba inatarajia kucheza mchezo
mwingine wa kirafiki siku ya Jumatano dhidi ya timu ya Manispaa ya
Kinondoni na kujiandaa kurudi Dar kwa ajili ya Simba day August 8.
PICHA MBALIMBALI KATIKA MCHEZO HUO;
Waamuzi katika mchezo huoKocha wa Bukinafaso Ulimboka Mwakingwe
Wachezaji wa Simba wakiteta jambo katika mchezo dhidi Bukinafaso
Mchambuzi wa michezo na mtangazaji wa Planet Fm 87.9 Morogoro,Mr Choi (kulia) akiteta jambo na msemaji wa 77 United iliyo daraja la pili mara baada ya mchezo wa Bukinafaso na Simba.
Mpiga picha wa gazeti namba moja la michezo Tanzania Championi, Omary Mdose akiwa makini kuchukua matukio ya mchezo kati ya Simba dhidi ya Bukinafaso .
Mchambuzi wa michezo na mtangazaji wa Planet Fm 87.9 Morogoro Mr'Choi (kushoto), akiwa na msemaji wa 77 United Abubakar Mkingie (katikati) pamoja na ripota wa Sports Xtra, Peter Andrew.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni