Simba SC leo wamecheza mchezo wa kirafiki na URA ya Uganda na mpaka dakika 45 za mwanzo zinamalizika ubao wa matokeo ulikuwaunasomeka kwa sare ya goli 1-1.
Katika mchezo huo uliojaa ufundi mwingi huku kila timu ikijaribu kutawala eneo la kati ya uwanja kwa kupokezana, na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga ambapo kila mmoja akitumia nafasi moja.
Walikuwa URA wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Nkugwa Elikana katika dakika 20 ya mchezo kabla ya Jonas Mkude kuisawaizishia Simba SC katika dakika ya 32 ya mchezo na kupeleka mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
Katika mchezo huo maalum ambao ulitumika kumuaga nahodha wa Simba SC Mussa Hassan Mgosi aliyetangaza kustaafu kucheza mpira na sasa atakuwa meneja wa timu hiyo, Mgosi alicheza kwa dakika 3 za mwanzo za mchezo na kumpisha Jamal Mnyate.
Dakika ya 69 Ajib alipata nafasi ya kuifungia Simba goli la pili baada ya kupokea pasi safi toka kwa Mavugo lakini shuti lake lilinyakwa na mlinda mlango Agaba Oscar.
URA walionekana kujilinda zaidi huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza lakini Simba walikuwa imara zaidi kuokoa hatari zote zilizokuwa zikijitokeza.
Simba iliwatoa Mgosi, Mnyate, Kichuya na Ajib nafasi zao zikachukuliwa na Musa Ndusha,Hajji Ugando pamoja na Fredrick Blagnon.
Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Vincent Angban, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hamad Juma, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shizza Kichuya/Hajji Ugando dk74, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo, Ibrahim Hajib/Frederick Blagnon dk79 na Mussa Mgosi/Jamal Mnyate dk3/Mussa Ndusha dk62.
URA FC; Oscar Agaba, Mathias Muwanga, Sam Sekito, Fahad Kawoya, Shafiq Kagimu, Jimmy Lule, Feni Ali, Labama Bokota, Julius Ntambi na Elkanah Nkugwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni