Katika raundi ya 4 ya mchujo wa kucheza hatua ya makundi ya michuano ya Europa League , Klabu ya KRC Genk anayokipiga mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania , Mbwana Samatta imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuza hatua ya makundi baada ya kutoka sare ya goli 2 – 2 na NK Lokomotiva ya Croatia .
Genk inanafasi nzuri ya kufuzu kutokana na kuwa na goli 2 za ugenini pale timu hizo zitakaporudiana wiki ijayo . Genk walianza kupata bao dakika ya 37 baada ya mchezaji wa Lokomotiva kuunawa mkono ndani ya box na kumfanya Leon Bailey afunge goli la kwanza la Genk .
Hadi Mpira unakwenda mapumziko , Genk ilikua inaongoza kwa bao 1 – 0 , ambapo dakika 2 baadae , Mtanzania Mbwana Samatta aliweza kuongeza bao la pili , baada ya kupokea krosi nzuri kutoka kwa Sandy Walsh na kuwafanya Genk waamini safari ya makundi kuwa imetimia .
Timu changa ya Lokomotiva haikutaka kukata tamaa mapema na kuendelea kupigana ambapo dakika ya 52 MirkoMaric aliifungia bao la 1 na dakika 7 baadae Ivan Fiolic aliweza kusawazisha kwa kufunga bao la pili .
Wiki ijayo , Tarehe 25 Agosti timu hizi mbili zitarudiana nyumbani kwa KRC Genk ambapo mechi hii ndio itaamua rasmi timu gani itasonga mbele kwenye hatua ya makundi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni