MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga leo wameachana rasmi na Mkurugenzi wao wa Ufundi, Mholanzi Hans van Der Pluijm.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali na kuthibitishwa na kocha huyo wa zamani wa Yanga, vinasema kuwa, timu hiyo imeachana rasmi naye.
Akithibitisha hilo Pluijm alisema Yanga wamemuandikia barua ya kukatisha mkataba wake kutokana na klabu hiyo kukumbwa na matatizo ya fedha.
"Ni kweli Yanga wamenipa barua ya kukatisha mkataba wangu na sababu kubwa ni kutokana na matatizo ya fedha yanayowakabili kwa sasa, “alisema Pluijm kwa kifupi.
Awali, Mholanzi huyo alitua Yanga kama Kocha Mkuu na baadae kuachana na timu hiyo kabla ya kurejea tena na kuwa kuendelea na nafasi yake.
Hata hivyo, Pluijm alikatisha mkataba wake baada ya Yanga kumchukua kocha wa Zesco ya Zambia, George Lwandamina kuchukua nafasi yake bila ya kumtaarifu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Mchemba alimshawishi Pluijm kurejea Yanga, lakini sasa akiwa Mkurugenzi wa Ufundi badala ya Kocha Mkuu.
Alisema kwa sasa hawezi kulizungumzia suala hilo, kwani yuko katika harakati za maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Mtibwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Alisema timu yao itaondoka kesho asubuhi kwenda Morogoro na jioni itafanya mazoezi kwenye uwanja huo uliofanyiwa ukarabati hivi karibuni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni