KAMATI ya utendaji ya klabu ya Yanga iliyokutana jana kwa dharura imetoa maazimio matano baada ya kutoalikwa kwenye hafla ya ugawaji vifaa vya michezo uliofanywa na wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom ikishirikiana na bodi ya ligi.
Uongozi wa mabingwa hao umesikitishwa na kitendo hicho cha kutopewa mwaliko wa hafla hiyo wakiwa ndio mabingwa watetezi kitu ambacho kiwachonganisha na mashabiki na wanachama hao.
Mjumbe wa kamati ya utendaji wa mabingwa hao Salum Mkemi amewaambia Waandishi wa Habari kuwa ilibidi kamati ya utendaji ikutane kwa dharura jana ili kujadili suala hilo na kutoka na maadhimio hayo.
Maazimio hayo ni kama yafuatavyo:
1. Bodi ya ligi, TFF na wadhamini watuandikie barua ili kutuomba radhi kwa kushindwa kutualika kwenye hafla.
2. Jezi zilizotolewa jana hazikutolewa na Vodacom bali zimetolewa na SportPesa kwahiyo Vodacom walifanya makosa kutangaza walitoa wao.
3. Tulipanga siku maalum ya kutambulisha jezi zetu kwa msimu wa 2017/18 na wadhamini wetu SportPesa watamleta beki wa zamani wa Arsenal, Sol Campbell ili kutambulisha jezi yetu, hivyo walichofanya Vodacom kimetupotezea mapato.
4. Klabu ya Yanga ipo tayari kupambana na mtu binafsi, kampuni au yoyote anayetaka kuhujumu mapato yetu.
5. Hatukupenda utani uliofanywa na Simba jana (Manara kuchukua zawadi kwa niaba yetu). Huu sio utani mzuri unaweza kuleta mgawanyiko ndani ya klabu hatutaki suala hili litokee tena.
CREDIT: BOIPLUS
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni