- etty
#1Kevin De Bruyne
Yawezekana isiwe haki, lakini zabuni ya De Bruyne katika mbio hizi unaweza kuathiriwa na ukosefu wa magoli. Utawala wa nyota wakuu wawili wa sasa umeimarishwa na umahiri wao wa kufunga - na kuwatengenezea wengine nafasi ya kufunga, lakini kufunga kwenye timu yenye mafanikio kunaongeza sifa. Angalau Mbelgiji huyo yupo kwenye klabu yenye mwelekeo thabiti kwani Manchester City inaweza kuwa klabu yenye nguvu zaidi chini ya uongozi wa Pep Guardiola. - Getty Images
#2Paulo Dybala
Dybala akiwa mchezaji muhimu Juventus kwa sasa, tumaini lake la Ballon d'Or kwa muda mrefu linaweza kutimia atakapoirithi nafasi ya Messi kwenye timu ya Argentina. Bado umri wake ni miaka 24 na hakuna sababu ya kupata hofu. Ameisaidia Binaconeri kutinga fainali Ligi ya Mabingwa msimu uliopitajambi lililompatia Dybala sifa na kukuza wasifu wake, na ameanza kampeni za Serie A kwa magoli 10 kwenye mechi sita. Ikiwa ataendeleza mwendo huo kwa kipindi kirefu, wapiga kura watalazimika kuanza kumpigia kura. - Getty
#3Eden Hazard
Hazard ameng'ara kwenye Ligi Kuu Uingereza akiwa na Chelsea, akiisaidia klabu kutwaa taji hilo mara mbili na pia kutajwa kwenye kikosi cha mwaka cha PFA mara nne katika misimu yakemitano Uingereza. Hata hivyo kwa ubora wake wote ndani ya fulana ya bluu, Mbelgiji huyo ameshindwa kuwashawishi wapiga kura wa Ballon. Akiendelea kuhusishwa na tetesi za kutua Real Madrid mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 atakuwa na hisia kuwa kutua Hispania kutazidi kuipandisha heshima yake kwenye soka. - Getty
#4Neymar
Wengi wanamtazama kama mchezaji bora wa tatu duniani kwa sasa, Neymar ni wazi kwamba yeye ndiye chaguo hapa. Mbrazili huyo alimaliza nafasi ya tatu 2015 na wa tano mwaka jana kabla ya kurejea tatu bora 2017, hayupo tena chini ya kivuli cha Messi Barcelona, kwa uhamisho wa rekodi ya dunia kwenda Paris Saint-Germain ili kuweza kupata mafanikio binafsi. Kwenda nje ya Hispania kutamfanya kuwa thabiti kushinda tuzo hiyo hata kama Ligue 1 inaonekana hatua moja chini ya La Liga. - Gettty
#5Kylian Mbappe
Mchezaji mwenzake Neymar PSG, kinda Mbappe ameibuka kwa kasi msimu uliopita aking'ara akiwa na Monaco na kwa haraka akahamia jiji kuu la Ufaransa. Alikiri mwezi Oktoba kuwa bado ana njia ndefu ili kuwa mshindani hasa wa Ballon d'Or, lakini mchezaji huyo mwenye kipaji ana muda mrefu kuliko majina yote yaliyoorodheshwa na wala si Messi na Ronaldo tu.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Alhamisi, 7 Desemba 2017
Home
/
Unlabelled
/
WAFAHAMU WACHEZAJI WATANO WANAOTARAJI KUWARITHI RONALDO NA MESSI KWENYE BALLON D'OR ZIJAZO
WAFAHAMU WACHEZAJI WATANO WANAOTARAJI KUWARITHI RONALDO NA MESSI KWENYE BALLON D'OR ZIJAZO
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni