STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 4 Desemba 2017

WAKATI DIRISHA LA USAJILI LIKIWA WAZI, SINGIDA UNITED LAWAPIGA PANGA NYOTA WAKE

Uongozi wa klabu ya Singida United ya mjini Singida umetangaza rasmi kuachana na wachezaji wanne Frank Zakaria, Atupele Green, Mohamed Titi na Pastrory Athanas.

Akithibitisha taarifa hizo Mkurugenzi wa Singida United Festo Richard Sanga amesema wameachana na washambuliaji Atupele Green na Pastory Athanas, wakati Frank Zakaria na Mohamed Titi wanapelekwa kwa mkopo Stand United.
Sanga amesema, wamewaacha wachezaji hao kwa madai ya changamoto ya ushindani wa namba, hivyo nafasi zao wanafikiria namna ya kuziziba.

-Atupele Green na Athanas wapo huru lakini Zakaria na Titi, tumewapeleka Stand United wakaangalie changamoto nyingine, ubora wa viwango vyao ndivyo vitakavyowarudisha kwenye timu, lakini pia muda huu tunatafuta wachezaji wa kuziba nafasi baada ya kuwaachia wachezaji hawa, "alisema Sanga.

Dirisha la usajili kufungwa. 
Hao wanakuwa wachezaji wa kwanza kutemwa na Singida United Huku Dirisha la usajili likiwa limebakiza siku 10 kufungwa na kupisha michezo ya ligi kuu soka Tanzania Bara inayotarajiwa kufikia tamati mwezi Mei mwakani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox