Stephen Keshi akiwa amebebwa alipotwaa ubingwa wa Afrika |
Shaibu Amodu anayemrithi Keshi kartika Super Eagles |
SHIRIKISHO la Soka la Nigeria, NFF, kimetangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha Mkuu wa Super Eagles, Stephen Keshi ikiwa ni saa chache tangu aiongoze timu hiyo kupata ushindi wa mabao 3-1 nyumbani dhidi ya Sudan katika mechi ya kuwania Fainali za Kombe la Afrika za 2015.
Kocha za zamani wa timu hiyo Shaibu Amodu ndiye aliyepewa mikoba ya kuuiongoza Super Eagles katika mechi zilizosalia za kundi lake.
Keshi, nyota wa zamani wa timu hiyo amekuwa kocha wa Nigeria tangu mwaka 2011 na alifanikiwa kuipeleka Super Eagles kwenye Fainali za Kombe la Dunia na kuishia nao raundi ya pili na inaelezwa tangu fainali hizo hakuwa na mkataba wowote licha ya kuendelea kuinoa timu hiyo aliyoipa ubingwa wa Afrika fainali za mwaka jana zilizofanyika nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa NFF, maamuzi ya kutimuliwa kwa Keshi yamekuja baada ya Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo kukutana jana.
"Kwa manufaa ya soka la Nigeria na kiu kubwa ya kushiriki fainali za mwaka 2015 kamati imeamua kuachana na Keshi na benchi lake lote la ufundi," taarifa ya NFF ilisomeka hivyo.
Badala ya keshi NFF imemtaja Amodu aliyewahi kuinoa timu hiyo katika vipindi vinne tofauti mara ya mwisho ikiwa ni mwaka 2008-2010.
Vipindi vingine ambayo Shaibu Amodu aliwahi kuiongoza timu hiyo ni mwaka 1994-95, 1998-99, 2001-2002, Mei Mwaka jana alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Soka nchini humo kabla ya kupata kazi kama hiyo katika klabu na kutema nafasi yake hadi alipoitwa leo na NFF kuwa Kocha Mkuu kwa mara ya tano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni