STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 30 Mei 2015

MBEYA CITY YAANZA KUJIJENGA BAADA YA KUBOMOLEWA, YASAJILI WAWILI

Beki wa kulia  Haruna Shamte aliyekuwa akicheza kwenye kikosi cha JKT Ruvu na kiungo mshambuliji wa Coastal Union, Joseph Mahundi  wamejiunga na Mbeya City fc wakiwa wachezaji huru.
Mapema leo kwenye ofisi za Mbeya City fc Mkapa Hall  katikati ya jiji la Mbeya  wachezaji hao wametia  saini kandarasi ya kucheza kwenye kikosi cha City  msimu ujao wa 2015/16, wakati Shamte akitia saini kandarasi ya mwaka mmoja, Joseph Mahundi amesaini  kandarasi ya mwaka mmoja na nusu  huku thamani ya kandarasi hizo ikibaki kuwa siri kwa mujibu wa makubaliano.
Mara baada ya kusaini kandarasi zao wachezaji hao wamesema kuwa  wamefurahi  kujiunga na timu ambayo kwa misimu miwili imekuwa bora  na kuleta changamoto kubwa kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara huku wakiahidi kufanya kazi kwa nguvu ili kuhakikisha City inapata mafanikio zaidi.
“Tofauti na watu wengi wanafikiri, binafsi naamini City ni timu nzuri na yenye malengo mazuri pia, nimefurahi kujiunga nayo kwa sababu najua naweza kupata mafanikio nikiwa hapa, tangu ilipopanda imekuwa na ushawishi mzuri kwenye ligi  hasa ukizingatia kuwa ni moja ya timu zenye wapenzi wengi hivi sasa, kikubwa tuombe mungu atupatie uzima, nataka kufanya kazi yangu kwa akili na  nguvu zote ili tupate mafanikio zaidi ya niliyoyakuta” alisema Shamte.
Kwa upande wake Mahundi  alisema kuwa, amefurahi kujiunga na timu ambayo  imekuwa ikicheza soka la ushindani mkubwa uwanjani jambo ambalo limeifanya kuwa sehemu ya timu nne za juu kwenye msimamo wa ligi kwa miaka miwili mfululizo.
“City ni timu nzuri imekuwa ikicheza soka la ushindani  na hii ndiyo sababu  imekuwa sehemu ya timu nne za juu kwa miaka miwili mfulilizo kwangu mimi hili limenifanya kuamini kuwa nikiwa hapa naweza kucheza michuano ya kimataifa, kuna timu nyingi zilihitaji huduma yangu lakini nimeamua kuchagua city kwa sababu hizo, unaweza usiamini lakini huo ndiyo ukweli, kuna baadhi ya timu zipo kwenye ligi miaka mingi lakini hazijawahi kuwa na ushawishi kama ilivyo timu hii” alisema Mahundi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa City Emmanuel Kimbe  amewashukuru wachezaji hao kwa kujiunga na timu, huku akiwahidi kufanya nao kazi kwa ushirikino zuri katika kuhakikisha mafanikio zaidi yanapatikana.
“Nawashukuru, mmejiunga nasi leo, nawakaribisheni sana, hii ndiyo timu ya kizazi kipya imani yangu mtafurahi zaidi, kwa niaba ya uongozi na  pia mashabiki wetu niwatoe shaka kuwa hapa mko sehemu  sahihi na tutafanya kazi kwa ushirikino mkubwa” alisema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox