KLABU ya Parma ya Italia imetangazwa mufilisi ambapo sasa inatarajiwa kuporomoshwa mpaka ligi daraja la nne maarufu kama Serie D.
Parma ilifanikiwa kumaliza katika nafasi ya nne katika msimamo wa Serie A msimu wa 2013-2014 lakini walijitoa katika michuano ya Europa League kutokana na mlolongo wa matatizo ya kifedha uliochangiwa kea kiasi kikubwa na suala la kubadili wamiliki.
Matatizo hayo yalichangia kwa kiasi kikubwa klabu hiyo kumaliza msimu wakiwa wanaburuza mkia katika msimamo wa Serie A msimu uliopita.
Kufuatia kushindwa kupata mmiliki mpya, mahakama iliitangaza mufilisi klabu hiyo huku wakishushwa daraja mpaka daraja la nne badala ya daraja la pili kama ilivyotakiwa kuwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni