BEKI wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, Eric Abidal ametangaza kuwa atakuwa mkurugenzi wa michezo wa Barcelona kama rais wa zamani wa klabu hiyo Joan Laporta atashinda katika uchaguzi unaokuja.
Abidal amewahi kuitumikia Barcelona kea kipindi miaka sita akishinda mataji manne ya La Liga na mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya mkataba haujamalika chini ya rais wa zamani Sandro Rosell.
Hata hivyo, Abidal mwenye umri wa miaka 35 sasa ametanza nia yake ya kurejea Camp Nou akiwa katika nafasi ya ukurugenzi akiwa katika kambi ya Laporta huku akijinasibu kuwa anataka kumtafuta Lionel Messi mwingine.
Barcelona kwasasa iko katika kinyang’anyiro cha kutafuta rais wake mpya baada ya Josep Maria Bartomeu aliyechukua nafasi ya Rosell aliyejiuzulu, kumaliza muda wake.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Julai 18 mwaka huu huku Laporta, Bartomeu, Agusti Benedito na Jordi Majo wote wakiwania nafasi hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni