STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 26 Agosti 2015

CAPITAL ONE CUP SPURS KUWA MWENYEJI WA ARSENAL,RATIBA KAMILI NIMEKUWEKEA HAPA....




Mabingwa wa kombe la FA, Arsenal watalazimika kuvuka mitaa na kuwafuata wapinzani wao wa Kaskazini mwa jiji la London Tottenham Hotspurs, kwa ajili ya kupambana kwenye mchezo wa mzunguko wa tatu wa kombe la ligi "CAPITAL ONE CUP"

Arsenal wameangukia kwa mahasimu wao  baada ya chama cha soka nchini Uingereza FA kuendesha zoezi la upangaji wa ratiba ya mzunguko wa tatu wa michuano hiyo ambayo huchezwa kwa mfumo wa mtoano.

Michezo mingine ya hatua ya tatu ya kombe la ligi ambayo inatarajiwa kuwa na mvuto pamoja na ushindani ni kati ya Aston Villa ambao watakua nyumbani Villa Park dhidi ya mahasimu wao wa jiji la Birmingham,Birmingam City.

Ipswich Town watalazimika kusafiri hadi mjini Manchester kwenye dimba la Old Trafford kupambana na Manchester United, Crystal Palace wakichuana na Charlton, wakati mabingwa watetezi Chelsea wakipangiwa kupambana na Walsall huko Bescot Stadium.

Klabu ya Carlisle inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Uingereza itakutana na majogoo wa jiji Liverpool kwenye uwanja wa Anfield, baada ya kufanya kazi kubwa ya kuichabanga Qpr mabao 2-1 katika mchezo wa mzunguko wa pili.

Kwa upande wa Manchester City wamepangiwa kukutana na Sunderland ambao watakua nyumbani Stadium of Light.

MICHEZO MINGINE:

Middlesbrough v Wolves Norwich v West Brom Hull v Swansea Leicester v West Ham Fulham v Stoke Newcastle v Sheffield Weds Reading v Barnsley or Everton Preston v Bournemouth MK Dons v Southampton


Michezo hii ya mzunguuko wa tatu imepangwa 

kuchezwa Septemba 22


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox