Bayern
 Munich walianza vyema kutetea ubingwa wao wa Bundesliga wakiifunga 5-0 
Hamburg SV kwenye mechi iliyopigwa Ijumaa iliyopita  uwanja wa Allianz 
Arena,  huku Thomas Muller akifunga magoli mawili.
Wakati
 huo huo, Manchester United walipata ushindi wao wa pili  kwa kushinda 
1-0 dhidi ya Aston Villa, ingawa bado hofu ipo  katika safu yake ya 
ushambuliaji.
Leo
 gazeti la The Sunday Express limeandika stori ukurasa wake wa nyuma 
akisomeka: "Thomas Muller anataka kujiunga na Manchester United,  hii ni
 kwa mujibu wa John Richardson.
Sunday
 Express wanaonekana kupata habari hiyo kutoka vyanzo makini vya masuala
 ya usajili vinavyodai Muller anataka kujiunga na mchezaji mwenzake wa 
zamani wa Bayern Munich aliyetimkia Old Trafford,  Bastian Schweinsteiger.
Hata
 hivyo, bosi wa Man United, Louis van Gaal bado hajakata tamaa 
kumfukuzia Muller, licha ya ofa yake kukataliwa. Dau la mwisho aliloweka
 mezani ni paundi milioni 60.
United wataendelea kujaribu kumsajili Muller na gazeti hilo pia limesema kwamba Van Gaal anamuwinda Gareth Bale.
Tazama ukurasa wa nyuma wa  Sunday Express, huku zikifuatiwa baadhi ya tweets juu ya tetesi hiyo.
 

 
 

 
 
 
 
 
 
 

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni