STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 11 Septemba 2015

DE GEA KUBAKI OLD TRAFFORD ASAINI MIAKA MINNE

GOLIKIPA wa Manchester United, David de Gea amesaini mkataba mpya wa miaka minne na klabu hiyo huku kukiwa na kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja zaidi. 

Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 24, ambaye alitua Old Trafford akitokea Atletico Madrid mwaka 2011 alikuwa akitegemewa kurejea La Liga kujiunga na Real Madrid kiangazi hiki. 

Hata hivyo, kufuatia uhamisho huo kushindikana katika siku ya mwisho kutokana na baadhi ya karatasi kuchelewa kufika, De Gea ameamua kusaini mkataba mwingine na klabu hiyo. 

Akihojiwa mara baada ya kusaini mkataba huo, De Gea amesema amefurahi kuanza ukurasa mpya katika maisha yake ya soka akiwa na United. 

Golikipa huyo aliendelea kudai kuwa kwasasa anataka kuachana na wakati mgumu aliopata majira ya kiangazi na kuanza kujituma kwa bidii ili aweze aweze kuisaidia United kupata mafanikio.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox