Staili ya mchezo wa kushambulia ya klabu ya Manchester United
imekuwa ikishambuliwa na wachambuzi wa michezo msimu huu lakini
hakukuwa na mashaka juu ya ubora wa pasi 45 zilizopigwa kabla ya
kufungwa kwa goli la tatu dhidi ya Southampton.
Goli hilo Juan Mata lilihakikishia United
ushindi muhimu lakini pia limewezq kuingia katika listi ya magoli
yaliyofungwa baada ya kupigwa kwa pasi nyingi katika kipindi cha miaka 5
iliyopita ndani ya Barclays Premier League.
Kabla ya kufungwa kwa goli hilo Manchester United
walipiga pasi 45, na hivyo kulifanya goli hilo kushika nafasi ya pili
kwa idadi ya pasi kabla ya goli huku nafasi ya kwanza ikishikwa na goli
la Nacer Chadli wa Tottenham aliyefunga goli dhidi ya QPR baada ya kupigwa kwa pasi 48.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni