Sir
Alex Ferguson ameweka wazi namna alivyokuwa akitawala kwenye klabu ya
Manchester United kwa kuhakikisha hakuna mchezaji ambaye analipwa pesa
nyingi kuliko yeye kwenye kipindi chake cha mwisho ndani ya Old
Trafford.
Ferguson
amesema aliiambia familia ya Glazer pamoja na mkurugenzi mkuu David
Gill kumuongezea mshahara wake mara mbili haraka iwezekanavyo baada ya
kufanya makubaliano ya kusainisha mkataba mpya mshambuliaji Wayne
Rooney kubakia Manchester United wakati alipokuwa akiwaniwa na
Manchester City mwaka 2010.
Kipengele
hicho kilikubaliwa bila kupingwa wala hakukuwa na tatizo katika hilo,
amefafanua kwenye kitabu chake kipya kinachokwenda kwa jina la
‘Leading’. Ferguson amesema aliendelea na utaratibu wa kuhakikisha
hakuna nyota wa klabu hio anaelipwa pesa nyingi kuliko kocha.
“Wakati
Glazer na Davi Gill walipokubali kuongeza mshahara wa Wayne Rooney,
waliniuliza najisikiaje juu ya hilo”, amesema Ferguson.
“Niliwaambia
sidhani kama inafaa Rooney kupata mshahara mara mbili ya ninaopata
mimi, Joel Glaze haraka akasema: “Moja kwa moja nakubaliana na wewe,
sasa tufanyaje?”
“Ilikuwa
rahisi. Tulikubaliana hakuna mchezaji atakakuwa akilipwa zaidi yangu.
Tukakubaliana ndani ya muda mfupi na inahitaji kusom sentensi iliyopita
kupata jibu”.
Rooney
alikuwa na miaka 24 wakati ule, miaka miwili ilibaki mkataba wake
kumalizika na ingeleta mkanganyiko wakati huo Manchester City walikuwa
wakimuhitaji.
Alitoa
kauli ambayo aliuliza malengo ya klabu wakati United walipokubali
kumlipa kiasi kikubwa cha mshahara kwa ajili ya kumbakiza.
Mshambuliaji huyo wa England alisaini mkataba mpya October 2010 wenye thamani ya mshahara wa £180,000 kwa wiki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni