STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 20 Septemba 2015

MNYAMA AUNGURUMA TAIFA, KIIZA AONDOKA NA MPIRA, AZAM, MTIBWA ZAUA

Hatrick ya kwanza katika ligi kuu ya vodacom msimu huu imefungwa leo katika ushindi wa Simba SC wa goli 3-1 mbele ya Kagera sugar, iliyofungwa na Hamiisi Kiiza katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa taifa hii leo.

Katika mchezo huo wa leo Simba SC waliuwanza mchezo kwa kasi ya kawaida sambamba na Kagera sugar ambapo kuilichukuwa dakika 20 bila ya kuwepo na shambulizi lolote  la maana kwa upande wote.


Katika dakika ya 31 Hamisi Kiiza aliiandika goli lake la kwanza katika mchezo huo wa leo kwa kichwa akiunga krosi ya Nimubona, goli lililo wapeleka mapumziko simba sc wakiwa na goli 1-0.


Kipindi cha pili Simba SC walirejie kwa kasi na kufanikiwa kuandika goli la pili katika dakika ya 46 kupitia kwa Amisi Kiiza, goli lililo waamsha Kagera sugar na kuanza kusaka magoli ya kusawazisha.


Katika dakika ya 50 Mbaraka Yusuf aliiandikia Kagera sugar goli pekee, ambalo lilieongeza kasi ya mchezo, huku pande zote mbili zikishambuliana kwa zamu.


Wakati mpira ukielekea mwishoni Hamisi Kiiza aliutumia vyema mpira aliotengewa na Mwinyi Kazimoto kuandika goli la 3 na kuipatia ushindi Simba SC wa goli 3-1.

Na kule Shinyanga
BAO pekee la Nahodha John Raphael Bocco limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Huo unakuwa ushindi wa tatu mfululizo kwa Azam FC inayofundishwa na Muingereza Stewart Hall, baada ya awali kushinda 2-1 dhidi ya Prisons Uwanja wa azam Comolex, Chamazi, Dar es Salaam na 2-0 dhidi ya Stand United Uwanja Kambarage, Shinyanga.

Azam FC sasa inashuka hadi nafasi ya tatu nyuma ya Simba SC, zikiwa na pointi sawa na Yanga SC, tisa kila moja, lakini zinazidiana kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa. 

Katika mchezo wa leo, Azam FC ilipata pigo baada ya Nahodha wake, Aggrey Morris kutolewa kwa kadi nyekundu, wakati mshambuliaji wa Mwadui FC, Rashid Mandawa alikosa penalti. 


Mechi nyingine za leo, Mtibwa Sugar imeshinda 2-1 dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro mabao yake yakifungwa na Salum Mbonde na Said Bahanuzi la wageni likifungwa na Kiggi Makassy, wakati Coastal Union imelazimishwa sare ya 0-0 na Toto Africans Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox