Baada ya kocha wa sasa wa klabu ya Manchester United Louis van Gaal
kusema kuwa mipango yake ya kustaafu soka baada ya miezi 18 ijayo iko
pale pale, wengi walianza kujiuliza maswali ni nani klabu ya Manchester United inamuangalia kama mbadala wake?
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 64 ambaye alisaini mkataba wa miaka mitatu wakati anajiunga na klabu hiyo ya Old Trafford mwaka 2014, maamuzi yake ni yale yale.
Wengi walikuwa wanatazamia baada ya kustaafu Louis van Gaal mwaka 2017, atakayekuwa mbadala wake ni Ryan Giggs ambaye ni kocha msaidizi wa klabu hiyo.
Stori kutoka mirror.co.uk ni kuwa mbadala wa Louis van Gaal baada ya kustaafu anatajwa kuwa sio Ryan Giggs ni kocha wa zamani wa klabu ya FC Barcelona ya Hispania na klabu ya FC Bayern Munich Pep Guardiola.
Van Gaal ambaye ametumia pound milioni 90 kusajili wachezaji makinda kama Anthony Martial, Luke Shaw na Memphis Depay inaripotiwa kuwa mpango wake wa kustaafu soka 2017 uko pale pale.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni