STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 16 Septemba 2015

PELLEGRINI AKATAA KUMLAMU STERLING......


MENEJA wa Manchester City, Manuel Pellegrini amekataa kumlamu Raheem Sterling kwa kipindi cha mabao 2-1 nyumbani kutoka kwa Juventus katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya jana. 

Sterling ambaye alijiunga na City akitokea Liverpool majira ya kiangazi amekuwa katika kiwango kizuri katika Ligi Kuu na kuisaidia timu hiyo kushinda mechi zao zote tano za ligi walichocheza.

Lakini Sterling ameingia katika utata baada ya kukosa nafasi mbili za wazi katika mchezo dhidi ya Juventus na baadae kujikuta akitolewa katika dakika ya 71.

 Akihojiwa Pellegrini amesema hadhani matokeo hayo waliyopata ni kwasababu ya makosa ya yaliyofanywa na Sterling. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa walimiliki mchezo huo vyema na hawakuwa na matatizo mengi ila katika soka mambo kama hayo ni ya kawaida. 

City watakuwa wakitegemea kupata alama katika mchezo wao unaofuata wa kundi D wakati watakapokwaana na Borussia Monchenglabach Septemba 30 mwaka huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox