Mshambuliaji wa zamani wa
Juventus na klabu za Manchester, Carlos Tevez ameomba radhi baada ya
kumvunja mguu mchezaji Ezekiel Ham wa Argentinos Juniors timu yake ya
Boca Junior ikiibuka mshindi wa mabao 3-1.
Tevez ambaye hakua na mchezo
mzuri siku hiyo aliwania mpira wa 50-50 na Ham na kusababisha kuvunjika
mguu kwa mchezaji huyo ambaye hata hivyo hakupewa adhabu yeyote kutokana
na tackling hiyo.
Tevez aliwahi haraka sana kuomba
msamaha kwa kilichotokea huku akionesha kusikitika kwake kwa kumrudisha
nyuma Ham. Lakini kocha wa Argentinos Junior amesema haamini kama kweli
Tevez hakukusudia kumuumiza Ham.
Tevez
amesema anajutia kwa maana alienda kwa ajili ya mpira huku akijitetea
kuwa hajawahi muumiza mtu yeyote katika career yake ya soka.
Tevez mwenye miaka 31 aliamua
kurudi nyumbani mara baada ya kuvichezea vilabu vya West Ham, Manchester
United na City pamoja na Juventus za barani Ulaya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni