STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 4 Septemba 2015

WENGER NI MUONGO,.... AZODOLEWA HADHARANI .........



Winga mahiri wa zamani wa klabu ya Arsenal ya Uingereza amefunguka na kusema kuwa kocha wa sasa wa klabu hiyo Arsene Wenger ni muongo. Paul Merson ambaye amewahi kukitumikia kikosi Arsenal katika miaka ya 90, ana mtuhumu kocha Wenger kuwa anadanganya mashabiki.

Klabu ya Arsenal ndio klabu pekee kati ya zile tano zinazo shika nafasi ya juu, ambayo haijafanya usajili wowote mkubwa zaidi ya kumsajili Peter Cech kutokea klabu ya ChelseaPaul Merson ana amini mashabiki wanahitaji kitu cha ziada ndani ya klabu ya Arsenal.

Arsene-Wenger-1716199
“Ana wadanganya mashabiki, mashabiki tunafikiri nini kinafuata? tunashuka kila wiki, tunalipa kwa gharama wachezaji halafu nini kinafuata? kushika nafasi ya nne? kiasi flani tuliweza kufanya vizuri katika kombe la FA tulilocheza Wembley.”>>> Paul Merson

“Kuna usemi katika maisha unasema ukiendelea kufanya unachofanya utapata matokeo yale yale kila siku. Ni vipi msimu huu utaenda kuwa tofauti kwa Arsenal? ni timu ile ile iliyomaliza msimu uliyopita ikiwa nyuma ya Chelsea kwa point 12, kwa nini tena msimu huu? itamaliza Ligi ikiwa mbele ya Chelsea?”>>> Paul Merson

Real-Madrid-vs-AS-Roma
” Kama nishabiki wa Arsenal ambaye unanunua ticket ya msimu, hizo ni fedha za mashabiki na sio za Arsene Wenger wala za klabu, ni fedha za mashabiki ambazo zinatumika kununua wachezaji”>>> Paul Merson

Winga huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza ana amini Wenger hakuwa na nia ya dhati ya kutaka kumsajili mshambuliaji chaguo lake la kwanza Karim Benzema, kwani kuuzwa au kuto uzwa kwa mchezaji huyo, mazingira aliyatengeneza yeye. Paul Merson ana amini kama Arsene Wenger angetoa pound milioni 75 Real Madrid isingeweza kukataa kumuachia Benzema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox