STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 8 Novemba 2015

SAMATTA, SAMATTA…NANI KAMA SAMATTA, AWAFUNGA TENA WAALGERIA, MAZEMBE YAUA 2-0 NA KUBEBA NDOO YA AFRIKA..........


IMG_20151108_181338

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amefunga bao moja na kuseti moja, TP Mazembe ikitimiza dhamira ya kutwaa ubingwa wa Afrika baada ya kuifunga 2-0 USM Alger ya Algeria.
 
Mchezo huo wa marudiano wa fainali ya Ligi ya Mabingwa uliofanyika Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, wenyeji walipata mabao yote kipindi cha pili.

 
Na Mazembe inatwaa taji la tano la Ligi ya Mabingwa kwa ushindi wa jumla wa 4-1, baada ya awali kushinda 2-1 mjini Algiers Jumapili iliyopita.
Samatta akipongezwa na Mtanzania mwenzake, Thomas Ulimwengu baada ya kufunga

Samatta leo aliwekewa ulinzi mkali na wachezaji wa USM hadi akalazimika kusubiri kufunga bao lake la saba katika michuano ya mwaka huu kwa penalti dakika ya 75, baada ya Rogger Asale kuangushwa.
  Samatta naye akamsetia pasi nzuri Assale kufunga bao la pili katika dakika za majeruhi baada ya kutimia dakika 90 za kawaida za mchezo.
  Matokeo hayo yanamfanya Samatta pia awe mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa msimu huu, baada ya kufikisha mabao saba.

IMG_20151108_181407
  Hii maana yake huu unakuwa mwaka wa pili mfululizo, Tanzania inatoa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa, baada ya mwaka jana Mrisho Khalfan Ngassa kuongoza pia akiwa na klabu ya Yanga SC, kabla ya kuhamia Free State Stars ya Afrika Kusini msimu huu.
  Ngassa alifunga mabao sita sawa na El Hedi Belameiri wa Setif, Haythem Jouini wa Esperance na Ndombe Mubele aliyekuwa AS Vita ya DRC, sasa Al Ahly.

IMG_20151108_181434
  Kikosi cha TP Mazembe kilikuwa; Muteba Kidiaba, Joel Kimuaki Mpela, Salif Coulibaly, Mbwana Samata, Adama Traore, Kissi Boateng, Solomon Asante/Rogger Asalle dk46, Thomas Ulimwengu/Daniel Adjei Nii dk90, Mikis Mina/Merveille Bokadi dk72, Boubacar Diarra na Yaw Frimpong.

IMG_20151108_190505
  USM Alger; Mohamed Zemmamouche, Arslane Mazari/Farouk Chafai dk51, Hocine El Orfi, Rachid Nadji, Houcine Benayada/Mohamed Amine Aoudia dk70, Nacereddine Khoualed, Hamza Koudri, Mokhtar Benmoussa/Ayoub Abdellaoui dk90, Brahim Boudebouda, Kaddour Beldjilali na Zinedine Ferhat.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox