Baada ya kucheza mechi 16, wamepoteza 9 na mpaka sasa wana pointi 15 tu – presha ya kumtimua kocha Jose Mourinho inazidi kupanda.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari leo mchana manejimenti ya timu inayoundwa na — Bruce Buck, Marina Granovskaia, Eugene Tenenbaum and Michael Emenalo — watakutana pamoja na Mmiliki Roman Abramovich kuamua hatma ya Mourinho.
Roman Abramovich itampasa aingie mfukoni na kumlipa Jose Mourinho kiasi kisichopungua £40million ikiwa menejimenti itaamua kumfukuza kazi leo Jumatano.
Wakati mreno huyo aliporejea katika klabu mwaka 2013, bodi ya menejimenti ilipiga kura 3-2 ili kumrudisha. Leo inaweza kuwa tofauti.
Kulipa fidia ya mkataba wa wake wa miaka minne unaomfanya alipwe £250,000 kwa wiki ni moja ya sababu kuu nyuma ya kusita kwa Chelsea kumtimua kazi Mourinho muda mfupi baada ya kusaini mkataba mpya.
Mourinho alikubali kuongeza mkataba mpya mwishoni mwa msimu uliopita lakini klabu ilisubiri mpaka mwezi August kabla ya kusaini mkataba mpya rasmi.
Baada ya kushinda ubingwa vizuri sana, Chelsea waliamini alikuwa kocha bora zaidi duniani na wakakubali kumuongezea mkataba wa miaka minne bila kukubaliana kuweka kipengele cha makubaliano endapo wakiamua kumtimua kazi. Sasa hivi endapo Abramovich atataka mreno aondoke itabidi amlipe fidia ya £40m – hii itakuwa mara ya pili Mourinho kulipwa fidia baada ya kufukuzwa na Chelsea.
Mwezi September 2007 Roman alimlipa Mourinho na staff wake £16m wakati alipomtimua kazi, lakini baadae alimtumia kocha huyo gari la Ferrari ikiwa kama shukrani kwa kazi aliyofanya.
WACHEZAJI WALIO TASMINIWA KAMA WANASTAHILI KUBAKI CHELSEA AU KESEPESHWA:
Thibaut Courtois
STAY
Asmir Begovic
STAY
Cesar Azpilicueta
STAY
Gary Cahill
STAY
Branislav Ivanovic
STAY
Baba Rahman
GO
John Terry
STAY
Kurt Zouma
STAY
Eden Hazard
JURY'S OUT
Cesc Fabregas
GO
Ruben Loftus-Cheek
STAY
Kenedy
STAY
Nemanja Matic
STAY
John Obi Mikel
GO
Oscar
GO
Pedro
GO
Ramires
STAY
Bertrand Traore
GO
Willian
STAY
Diego Costa
GO
Radamel Falcao
GO
Loic Remy
STAY
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni