MSHAMBULIAJI
wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang ameonyesha kutoelewa
kauli ya Yaya Toure aliyotoa kufuatia kushindwa katika tuzo ya mchezaji
bora wa mwaka wa Afrika.
Kiungo huyo wa Manchester City alikuwa na
matumaini ya kushinda tuzo hiyo kwa mara ya tano mfululizo lakini
alizidiwa na Aubameyang ambaye amekuwa na rekodi nzuri ya ufungaji
katika Bundesliga.
Toure alimpongeza nyota huyo mwenye umri wa miaka 26
lakini pia alikandia suala la upigaji kura lilivyofanyika akidai
linaitia aibu bara la Afrika.
Akihojiwa Aubameyang amesema hafahamu
kwanini Toure aliongeza maneno hayo na hawezi kuchukia kuhusu hilo kwani
kwa upande wake tayari habari hiyo imeshapitwa na wakati.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni