Wakati mambo yakiwa hayawaendei sawa katika msimu huu, klabu ya Real Madrid ya Hispania imepokea taarifa mbaya zaidi katika mikakati yake ya kujiimarisha.
Real Madrid na mahasimu wao Atletico Madrid leo wamepokea hukumu yao ya kufungiwa kusajili wala kuuza mchezaji yoyote ndani kwa vipindi viwili vya usajili vijavyo .
Klabu hizo zimeadhibiwa na shirikisho la soka duniani Fifa kwa kukiuka sheria za uhamisho wa wachezaji kuhusu kununuliwa kwa wachezaji ambao bado ni watoto. .
Adhabu hii inatokana na makosa ya kusajili wachezaji walio chini ya umri kama ilivyokuwa kwa FC Barcelona.
Chama cha soka cha Spain (RFEF) kimekuwa kikusanya taarifa zote kuhusu wachezaji walio chini ya umri wa kisheria waliopo katika vilabu hivi viwili.
Walikuwa na mashaka juu ya vilabu hivi kuvunja sheria namba 19, inayokataza uhamisho wa wachezaji walio chini ya miaka 18 ambao hawana ruhusa rasmi ya vigezo maalum.
Takribani wachezaji 50 katika vilabu hivyo walikuwa wakichunguzwa, na inaripotiwa kwamba kwa kufahamu kwamba wanaweza kukumbwa na mkono wa sheria Los Blancos wakafanya haraka kukamilisha usajili wa Marco Asensio, Jesus Vallejo na Martin Odegaard.
Marufuku hiyo haitaathiri kipindi cha sasa cha kununua wachezaji, ambacho kinaendelea hadi mwisho wa mwaka huu.
Atletico pia wametozwa faini franka 900,000 za Uswizi ambazo ni sawa na pauni 622,000 za Uingereza, nao Real wakatakiwa kulipa franka 360,000 (£249,000).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni