MSHAMBULIAJI
Mario Balotelli sasa milango iko wazi kutua Arsenal baada ya wakala
wake kusema kwamba 'chochote kinawezekana' katka dirisha hili la
usajili.
Mpachika
mabao huyo wa Italia, aliyefunga bao la ushindi dhidi ya England katika
Kombe la Dunia Jumamosi iliyopita, yumo kwenye orodha ya wachezaji
wanatakiwa na kocha Arsene Wenger.
Arsenal
imewasiliana na wakala wake, Mino Raiola katika harakati za kutaka
kumng'oa mshambuliaji huyo AC Milan na wakala huyo hajakataa.
Anaweza
kuhamia Emirates: Wakuu wa Arsenal wanaamini wanaweza kumpata
Balotelli katakana na AC Milan kutaka kupunguza bajeti yao ya mishahara
"Arsenal
ni klabu nzuri,"amesema wakala wa Balotelli, Mino Raiola akihojiwa na
Sky Sports. "Atahamishwa? Chochote kinawezekana,".
Arsenal intake kwanza kujua gharama za kumsajili Balotelli kabla ya kuanza jitihada rasmi za kumnunua. AC Milan iko tayari kumtoa mchezaji huyo mtata, kwa sababu wanataka kupunguza bajeti yao ya mishahara msimu ujao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni