Furaha bab kubwa!: Wachezaji wa Brazil
wakishangilia ushindi wao wa penati 3-2 dhidi ya Chile na kufanikiwa
kufuzu hatua ya robo fainali.
WENYEJI Brazil wamekuwa wa kwanza
kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe la dunia baada ya jana usiku
kuifunga Chile kwa mikwaju 3-2 ya penati kufuatia sare ya bao 1-1 katika
dakika 90 za kawaida na dakika 30 za nyongeza.
Kutokana
na matokeo hayo, baadhi ya wachambuzi wa soka wameanza kuwa na wasiwasi
na mwendo wa Brazil na kushindwa kutambua watafika hatua gani.
Lakini sapoti kubwa wanayopata kutoka kwa mashabiki wao inaweza kuwa motisha kubwa kwao na wakajikaza hatua inayofuata.
Jibu
ni rahisi, yawezekana wakafika fainali na kutwaa ubingwa wao wa sita wa
kombe hilo , lakini ukweli unabaki palepale kuwa wanahitaji kukaza
sana.
Chile walicheza mpira mzuri na kuwabana Brazil kwa kila namna mpaka waliposubiri hatua ya mikwaju ya penati.
Gonzalo
Jara aliyecheza Nottingham Forest msimu uliopita ndiye alikosa penati
ya tano na ya mwisho kwa Chile. Mkwaju wake uligonga mwamba na baada ya
hapo Taifa zima la Brazil lilipuka kwa shangwe, nderemo na vifijo
wakishangilia ushindi.
David Luiz akishangilia baada ya kufunga penati yake dhidi ya Chile
Mashujaa wa Brazil , Julio Cesar na David Luiz wakikumbatiana kwa furaha baada ya kushinda
Neymar akijitahidi kuzuia hisia zake za machozi kwa kumkumbatia bosi wake Luiz Felipe Scolari
Wachezaji wa Chile wakiwa na huzuni baada ya kutolewa katika mikwaju ya penati
Mikwaju ya penati baina ya Brazil dhidi ya Chile
1-0 BRAZIL: David Luiz - alifunga1-0 BRAZIL: Panilla - alikosa -Kipa alidaka
1-0 BRAZIL: Willian - alikosa - alipiga nje upande wa kushoto
1-0 BRAZIL: Sanchez - alikosa - Kipa alidaka
2-0 BRAZIL: Marcelo - alifunga
2-1 BRAZIL: Aranguiz - alifunga
2-1 BRAZIL: Hulk - alikosa - Kipa aliokoa
2-2: Diaz - alifunga
3-2 BRAZIL: Neymar - alifunga
3-2 BRAZIL: Jara - alikosa-iligonga mwamba
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni