STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 6 Juni 2014

GEBO PETER KUZIKWA KESHO KIGURUNYEMBE

Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam Gabriel Peter Magali, maarufu kama Gebo Peter atazikwa kesho kijijini kwao, Kigurunyembe mkoani Morogoro.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa taarifa ya kuupokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji mrefu, aliyekuwa mkali wa kufunga mabao ya vichwa enzi zake.
Gebo ambaye pia kama kaka yake Agustino Peter ‘Peter Tino’  alichezea timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ameaga dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) mjini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwamatibabu.
 


Marehe Gebo enzi za uhai wake

Gebo aliyezaliwa mwaka 1961, pia aliwahi kuchezea timu za Sigara ya Dar es Salaam, CDA ya Dodoma na kombaini ya Mkoa wa Dar es Salaam (Mzizima United). Hadi mauti yanamkuta alikuwa akijishughulisha na biashara, kubwa ikiwa ya vifaa vya michezo.
Kwa sasa, msiba upo nyumbani kwao Vingunguti karibu na Kanisa Katoliki, Dar es Salaam ambapo taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na familia.
Marehemu ambaye ameacha mjane na watoto watatu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox