STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 4 Juni 2014

HANS POPPE: MSITUMIE JINA LANGU VIBAYA, MIMI NI SIMBA DAMU NA SIWEZI KUITUPA TIMU YANGU

MFADHILI na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amewaasa Waandishi wa Habari katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa klabu hiyo kuacha kuandika habari za upotoshaji.
Hans Poppe amesikitishwa na habari zilizoandikwa na gazeti moja la michezo leo, zikimnukuu akisema kwamba hataki kujihusisha na masuala ya usajili, badala yake ataelekeza nguvu zake katika biashara zake.
“Huyu mwandishi kweli nilizungumza naye, lakini amekwenda kuandika vile ambavyo anataka yeye, na si kutokana na mazungumzo yetu, sasa hii ni kitu hatari sana na kwa kweli sipendi,”alisema Hans Poppe.
Mfadhili na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe 

Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) amesema si mara ya kwanza kwa waandishi wa gazeti hilo kuzungumza naye na kwenda kuandika tofauti- na haelewi lina mlengo gani.
“Itafika wakati mtu sasa utaogopa kuzungumza na Waandishi wa Habari, ikiwa unachozungumza sicho kinachokwenda kuandikwa. Nilichosema mimi ni kwamba, siwezi kuingia Mkataba na mchezaji kwa sasa, kwa sababu sielewi uongozi utakaoingia madarakani utakuwa ni upi na kama utakubaliana na usajili huo au la,”.
“Maana unaweza ukaingia mkataba na mchezaji kwa sasa, halafu uongozi utakaoingia madarakani uwe wa yeyote yule, ukamkataa, utakuwa umemuingiza mchezaji na klabu pia kwenye matatizo,”.
“Lakini, ninachoendelea kufanya kwa sasa ni kuzungumza na kufikia makubaliano na wachezaji ambao kocha (Zdravko Logarusic) amewapendekeza, ili uongozi mpya ukiingia madarakani, niupelekee mapendekezo hayo, wakiafiki basi ni uongozi huo mpya ndiyo utakuwa umeingia mikataba na hao wachezaji,”alisema Poppe na kuongeza;
“Lakini Mwandishi kaenda kuandika habari tofauti kwamba mimi sitaki kusajili najihusisha na biashara zangu tu, na labda Wambura (Michael, mgombea Urais) ataingia madarakani, biashara zangu zipo siku zote na bado nimeendelea kufanya shughuli za Simba SC kwa mapenzi yangu kama mwanachama,”.
“Na uongozi wowote utakaoingia madarakani una haki ya kuwa timu wanayoitaka wao, hivyo si busara kuwasajilia wachezaji, ambao pengine hawatawataka, na vile vile Wambura kwa upande wake akifanya kampeni kabla ya wakati, amekwishaweka wazi kwamba, akiingia madarakani atawafukuza wachezaji wote waliopo sasa, katika hali hii ukiingia Mkataba na mchezaji yeyote kitatokea nini?,”alihoji Poppe.
Poppe amesema kwamba yeye ana mapenzi ya dhati ya Simba SC na hawezi kuitupa klabu hiyo, isipokuwa tu pale atakapoona uongozi unakwenda ovyo.
 “Huwezi kuiacha Simba SC kwa sababu ya mtu, ila kama wanaingia madarakani viongozi ambao unaona kabisa hawa wapo pale kwa maslahi yao binafsi na si maslahi ya klabu, hao huwezi kushirikiana nao,”amesema.
Hans Poppe amerudia kuwakumbusha wanachama wa Simba SC kuwa makini kuelekea uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo mwishoni mwa mwezi huu kwa kuchagua viongozi ambao watairudisha klabu katika mstari.
 “Kama ambavyo unaweza kuona kwa sasa, klabu yetu imepoteza mwelekeo kwa sababu ya uongozi ambao ulikosa mshikamano, sasa hatutakiwi kurudia makosa,”amesema. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox